
CLUBS
KLABU YA WATOTO
(Kids' Club)
Klabu hii ni ya watoto wa umri kati ya mwaka mmoja (1) mpaka miaka kumi na miwili (12). Watoto hawa hukutana mara moja kwa mwaka (wakati wa kiangazi) kwa lengo la kufahamiana, kujifunza mila na desturi za kitanzania na kimarekani, na pia kucheza pamoja. Klabu hii ni muhimu sana katika kujenga msingi wa udugu na ushirikiano kwa watoto wenye asili au nasaba ya kitanzania.

KLABU YA WANAWAKE
(Women's Club)
Klabu hii ni mahsusi kwa wanachama wanawake waliojiunga kwa lengo la kufahamiana, kubadilishana mawazo, na kushirikiana katika shughuli na mipango mbalimbali ya maendeleo waliyojipangia. Wanawake walio wanachama wa TSA tu ndio wanaoruhusiwa kikatiba kujiunga na klabu hii.

KLABU YA BURUDANI
(Entertainment Club)
Klabu hii hushughulika na maandalizi ya sherehe ya chama (TSA) inayofanyika kila mwisho wa mwaka (mwezi Desemba). Sherehe hii huhusisha wanachama wote wenye umri kuanzia miaka ishirini na mbili (22) kwenda juu. Klabu pia iko tayari kusaidia shughuli za mwanachama yeyote anayeomba kusaidiwa.

KLABU YA VIJANA
(Teens' Club)
Klabu hii ni ya vijana wenye umri kuanzia miaka kumi na tatu (13) hadi ishirini na moja (21). Vijana hawa hukutana mara kwa mara kwenye mtandao wa ZOOM kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kijamii. Aidha kila mwaka mnamo majira ya kiangazi vijana hukusanyika pamoja kufahamiana, kucheza pamoja, na kujifunza mila na desturi za kitanzania na kimarekani.
_edited.jpg)
KLABU YA WANAUME
(Men's Club)
Klabu hii ni ya wanaume waliokubali kuungana kwa lengo la kufahamiana, kubadilishana mawazo, na kufanya mambo mbalimbali ya kijamii kwa kadri ya makubaliano yao chini ya muongozo wa katiba ya TSA. Klabu hii inapokea wanachama wa TSA tu.

KLABU YA UWEKEZAJI
NA BIASHARA
(Investments Club)
Klabu hii ni ya wanachama walioamua kujiunga kwa lengo la kuinuana kiuchumi. Wanachama wanao mfuko maalum (unaojitegemea) waliouanzisha kwa lengo la kuinuana katika biashara na uwekezaji. Wanachama pia wana mpango wa kuanzisha kitega uchumi cha pamoja .

KLABU YA RAHA
(Enjoyment Club)
Klabu hii ni ya wanachama wanaopenda kujiunga kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kwa mujibu wa sheria walizojiwekea. Wanachama hujumuika mara kwa mara kufurahi pamoja kwenye sherehe mbalimbali hususan harusi, baby showers, birthdays, bridal showers na kadharika.

KLABU YA BIMA
(Insurance Club)
Klabu hii bado iko katika hatua ya maandalizi, hivyo haijaanza kufanya kazi. Maandalizi yatakapokamilika klabu hii itashughulika na masuala ya bima mbalimbali kwa ajili ya wanachama watakaopenda kujiunga. Kwa maelezo zaidi wasiliana na viongozi wa TSA.
