1st Youth & Teens Gala
- TSA HOUSTON

- Jun 20, 2022
- 1 min read

Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki,
Napenda kuwataarifu kuwa tunaandaa 1st Youth & Teens Gala itakayofanyika tarehe 16 Julai 2022. Gala hii kama jina linavyojieleza, ni kwa ajili ya vijana wa umri kuanzia miaka kumi na mitatu (13) hadi ishirini na minne (24). Lengo ni kuwakutanisha vijana ili waweze kufahamiana, na kujadili mambo mbalimbali yanayowakabili katika makuzi yao.
Tunaomba ushirikiano wenu wa hali na mali ili kufanikisha Gala hii. Wazazi wenye vijana wenye umri uliotajwa hapo juu, tafadhali wafahamisheni kuwa hii ni shughuli yao, na imeandaliwa kufuatia malalamiko yaliyokuwa yamejitokeza siku za nyuma. Ni wazazi wachache tu watakaoshiriki kwa ajili ya kuratibu, kushauri, na kujibu maswali yatakayojitokeza.
Tafadhali saidia kufanikisha Gala hii kwa kuchangia kiasi kidogo cha fedha kwa kadri utakavyojaliwa. Waswahili husema "haba na haba hujaza kibaba." Unaweza kutuma mchango wako kupitia namba zifuatazo:
Cashapp:
832 541 2554
$CMZ0221
Zelle:
832 884 4222
Rose Lupiana
Ahsanteni,
Mungu awaongezee mtakapotoa.
Rose Lupiana
Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa TSA


Comments