Shukrani za Dhati
- TSA HOUSTON

- Aug 5, 2023
- 1 min read
Mabibi na Mabwana,
Kwa niaba yangu binafsi na uongozi mzima wa TSA napenda kutoa shukrani za dhati kwa vijana wa TSA, viongozi wa TSA Teens Club, wanachama wa TSA, wazazi na wafadhili wote mliofanikisha Sauti za Afrika TSA Gala kwa hali na mali. Shukrani za pekee ziende kwa wageni wetu mliokubali mualiko wa kuhudhuria, na wazazi kwa kuwaruhusu vijana wenu kuwa sehemu ya siku hiyo muhimu. Uwepo wa vijana wenu ndiyo uliofanya shughuli hii ifanyike kwa mafanikio makubwa.
Vijana wamejifunza mengi kutoka kwa wazazi, wageni rasmi, na kwa kubadirishana mawazo wao kwa wao. Suala kubwa lililotiliwa mkazo katika shughuli hii ni jinsi watoto wetu wanavyoweza kupambana na changamoto za shule na vyuo wanavyosoma hususan suala la afya ya akili, madawa ya kulevya na nidhamu ya maisha. Vijana wamefurahia na kupokea ushauri waliopewa.
Nawashukuru sana, na Mungu awabariki.
Rose Lupiana
Rais & Mkurugenzi Mtendaji


Comments