Shukrani za Dhati toka TSA
- TSA HOUSTON

- Jul 20, 2022
- 1 min read
Updated: Sep 3, 2022
Mabibi na Mabwana,
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa TSA/TSA Teens Club, wanachama wa TSA, wazazi na wafadhili wote mlioweza kuchangia shughuli ya vijana wetu. Nawashukuru pia wazazi mlioweza kutuwakilisha, na kuleta vijana wenu kwenye shughuli hii. Uwepo wenu na wao ndio uliofanikisha shughuli nzima. Namshukuru pia kila mtu mmojamoja aliyeshiriki kwa hali na mali kuhakikisha 1st Youth & Teens Gala inafanikiwa.
Vijana walijifunza mengi kwa kutoa maoni yao mbalimbali kuhusiana na malezi/changamoto wanazopitia kama vijana. Baadhi yao walielezea ujuzi wao, vipaji na biashara wanazozifanya nje ya shule na kazi zao. Kwa ujumla vijana walifurahi sana.
Tutakuwa na mazungumzo baina ya wazazi na vijana tarehe 10 Desemba kujadili mambo mengine yenye manufaa kwa vijana wetu. tunawakaribisha wote mtakaoweza kushiriki.
Tunawashukuru sana, na Mungu awabariki.
Rose Lupiana
Mwenyekiti & Mkurugenzi Mtendaji


Comments