Shukrani za Dhati - Toka Uongozi wa TSA
- TSA HOUSTON

- Jun 15, 2022
- 1 min read
Mabibi na Mabwana,
Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa TSA/TSA Kids Club, wanachama wa TSA, wazazi na wafadhili wote walioweza kuchangia shughuli ya watoto wetu. Nawashukuru pia wazazi walioweza kuleta watoto kwenye shughuli hii, kwani uwepo wao ndio uliofanikisha shughuli nzima. Namshukuru pia kila mtu mmoja mmoja aliyeshiriki kwa hali na mali kuhakikisha TSA Kids & Friends Event inafanikiwa.
Tulianza kwa kujifunza kuchora na kupaka rangi bendera ya Tanzania na Marekani (painting). Baadae watoto walionesha ujuzi na vipaji vyao katika michezo na sanaa mbalimbali. Siku zijazo tutawaonesha/kuwashirikisha kazi za sanaa walizozifanya, na kuwaomba mtuunge mkono kwa kuzinunua.
Kwa ujumla watoto walifurahi sana, na wangependa kuendelea kucheza michezo mingi zaidi. Lakini kwa kuwa muda ulikwisha, wametupatia michezo hiyo ili tuwaandalie katika shughuli ya mwakani.
Tunawashukuru sana, na Mungu awabariki.
Rose Lupiana
(Mwenyekiti & Mkurugenzi Mtendaji wa TSA).


Comments